Mlipuko wawaua watu 11 Baghdad

Haki miliki ya picha epa
Image caption Iraq

Mashambulizi ya mabomu yamewaua takriban watu 11 katika wilaya zenye washia wengi kwenye mji mkuu wa Iraq Baghdad.

Magari yaliyokuwa yametegwa mabomu yalilipuka wakati watu walipokuwa wakifungua siku ya mwezi mtukufu wa ramadhan.

Haijabainika yule alitekeleza shambulizi hilo lakini utawala nchini Iraq unawalaumu wanamgambo wa Islamic state kwa mashambulizi yote ya karibu kila siku mjini Baghdad.