Watawa wakataa kumuuzia nyumba Katy Perry

Image caption Katy Perry

Mpango wa Katy Perry wa kutaka kununua jumba moja la watawa wa kikatoliki umepingwa na watawa waliokuwa wakiishi katika jumba hilo.

Msanii huyo nyota anataka kununua nyumba hiyo ilio juu ya mlima ambapo unaweza kuiona milima ya San Gabriel mjini Carlifornia ambayo ilikuwa makaazi ya Sister of the Immaculate Heart of Mary.

Alikubaliana kulinunua jumba hilo kwa kitita cha dola milioni 14.5 na kanisa la Los Angeles.

Hatahivyo watawa hao walisema kuwa nyumba hiyo ni yao na waliiuza kwa wamiliki wa mkahawa wa Dana Hollister wiki mbili zilizopita.

Image caption Jumba la watawa lililokuwa linunuliwe na katy perry

Wakati watawa hao walipokutana na Katy Perry hawakujua kuhusu muziki wake ambao unashirikisha nyimbo kama vile 'as I kissed a girl','Ur so Gay' na 'By the Grace of God'.

Lakini walimchunguza katika mtandao wa internet na hawakufurahia matokeo yake.

''Niliona kanda zake za video na sikufurahishwa Sister Rita Callana aliliambia gazeti la Los Angeles Times''.