Tishio kwa uhuru wa kujieleza Misri

Haki miliki ya picha AP
Image caption Wanamgambo kutoka Sinai wametekeleza mashambulio dhidi ya serikali

Sheria hiyo itawazuia waandishi kutoa taarifa inayokwenda kinyume na taarifa ya serikali kuhusu mapigano na wanamgambo.

Wiki iliyopita, kulishuhudiwa mashambulio mawili makuu ya wanamgambo dhidi ya serikali.

Mwendesha mashtaka mkuu aliuawa mjini Cairo, na kufuatia na shambulio moja siku mbili baadaye, dhidi ya vikosi vya serikali lililotekelezwa na wapiganaji jihadi wanaoshirikiana na Islamic State kaskazini mwa Sinai.

Haki miliki ya picha AP
Image caption Mwendesha mashtaka Hisham Barakat aliuawa katika mojawapo ya mashambulio

Taarifa zinaashiria kwamba vikosi vya serikali vimeshambuliwa pakubwa na kusababisha vifo vya hadi wanajeshi sitini.

Lakini idadi rasmi ilikuwa chini. Sheria hiyo mpya dhidi ya ugaidi ilipitishwa bungeni siku ya shambulio, lakini bado rais anahitaji kuiidhinisha.

Iwapo ingekuwa imeidhinishwa, mwandishi yoyote atakayetangaza idadi isiyo ya serikali huenda angekuwa anakabiliwa na kifungo cha miaka miwili gerezani.