Facebook imechangia ongezeko la talaka China

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Maafisa nchini Uchina wanaulaumu mtandao wa kijamii wa Facebook kwa ongezeko la idadi ya talaka nchini humo.

Shirika la habari la serikali nchini Uchina limeripoti ongezeko la wanandoa wanaotengana kufuatia matumizi ya kupita kiasi ya mtandao wa facebook.

Afisa huyo anasema kuwa ongezeko la watu wanaotumia mtandao huo wa umechagia kuongozeka kwa idadi ya watu wanatalikiana.

Yamkini ndoa nyingi zinavunjika kwani wachumba wanatumia muda wao mwingi wakiwa kwenye mtandao wa facebook na hivyo wanawatenga wapenzi wao ambao mwishowe huhisi wanatengwa na kuamua kuonja asali ya nje ya ndoa.

Kulingana na takwimu za serikali idadi ya watu wanaotoa talaka imeongezeka maradufu katika kipindi cha miaka kumi iliyopita.

Sababu zingine zinazotolewa kwa ongezeko hilo la talaka, ni kuwepo kwa njia rahisi ya kutoa talaka.

Haki miliki ya picha THINKSTOCK
Image caption Kulingana na takwimu za serikali idadi ya watu wanaotoa talaka imeongezeka maradufu

Aidha wakuu wanalaumu talaka bandia ambayo ni mbinu ya wapenzi wanaopanga njama ya kutengana rasmi ilikuepuka malimbikizi ya kodi na kisha wanaoana tena.

Wanandoa wengine hutumia talaka kama njia ya huepuka masharti makali ya kuthibiti kuwepo kwa nafasi za kazi na pia nafasi za kupata masomo.