Muda unayoyoma kwa mazungumzo ya Iran

Haki miliki ya picha EPA
Image caption Makubaliano yanatarajiwa kufikiwa ifikapo Julai 7.

Mawaziri wa mambo ya nje kutoka mataifa sita yenye nguvu duniani yanayohusika katika majadilianao hayo wanatarajiwa kuwasili Vienna kusaidia kufikiwa makubaliano hayo.

John Kerry alifungua jukwaa kwa shinikizo kubwa la kufikia muda wa mwisho uliotolewa kufikiwa makubaliano hayo ambayo ni tarehe 7 mwezi Julai.

Amesema kumepigwa hatua, lakini washiriki wa majadiliano hayo bado hawajaafikiana kuhusu masuala magumu zaidi.

Haki miliki ya picha US DEPARTMENT OF STATE
Image caption John Kerry asema huenda bado mazungumzo yasifanikiwe.

Na iwapo maamuzi magumu yatafikiwabasi huenda makubaliano hayo yakafikiwa wiki hii. Na iwapo maamuzi hayo hayatopitishwa hakuna makubaliano yatakayo fikiwa.

Ametangaza kwamba rais Barack Obama bado yupo tayari kuondoka katika meza ya mazungumzo iwapo Iran itakataa kubadili msimamo wake.

Pande zote zinataka mafanikio- ambayo kwa Iran itamaanisha kuondolewa vikwazo ilivyoidhinishiwa, na kwa washirika wake kwenye majadiliano hayo, itafanikiwa kuidhinisha vikwazo vikali kwa uwezo wa Iran kuunda bomu la nyuklia.