Uzazi wa upasuaji kupunguzwa Brazil

Haki miliki ya picha THINKSTOCK
Image caption Wanawake wengi huamua kufanyiwa upasuaji kukwepa uchungu wa uzazi

Sheria hizo mpya zinawalazimu madaktari kuwaarifu wanawake kuhusu hatari zilizopo na pia kuwashurutisha watie saini fomu za idhini yao kabla ya kuwafanyia upasuaji huo wakati wa kujifungua.

Madaktari hao pia watahitajika kutoa rekodi ya kujifungua kwa akina mama na kubainisha ni kwanini ilibidi wafanyie upasuaji.

Wanawake wengi Brazil hupendelea kuzaa kupitia upasuaji.

Katika hospitali za umma wanawake huona ndio njia salama na kwa walio na uwezo, wao huamua kuwalipa madaktari kando, kukwepa kukabiliwa na saa kadhaa za uchungu wa uzazi katika hospitali zilizo jaa wagonjwa.

Wanawake walio tajiri wanaokwenda katika hospitali za kibinafsi, wanaona upasuaji wakati wa uzazi ndio njia ya kisasa ya kujifungua.