Je video ya Rihanna ni 'Chafu' au inatisha?

Haki miliki ya picha afp
Image caption Je video ya Rihanna ni 'Chafu' au 'inatisha'?

Mwanamuziki wa chapa ya Pop, Rihanna ametibua mjadala mkali sana kwenye mitandao ya habari za Muziki na wasanii.

Hii ni baada ya kipusa huyo kuachia video yake mpya ya dakika 7 siku tano zilizopita ambayo inapongezwa kwa usanii na vilevile inakashifiwa sana kwa kuonyesha viungo vya utu uzima na kuwa na fujo kupita kiasi.

Aidha wanaoikashifu wanadai kuwa inaonesha unyama na ukatili wake ambayo wanahofu itawapotosha wafuasi wake wanaomtazamia kuwapa mwelekeo.

Katika video hiyo Rihana anaonekana akimlewesha mwanamke ambaye mumewe inakisiwa anadeni lake.

Haki miliki ya picha Getty
Image caption Video hiyo ya Rihanna imetazamwa na watu milioni 17 katika siku 5 tu

Muimbaji huyo baadaye anachukua kisu na kisha video inakamilika akiwa ametulia kwenye kasha lililojaa pesa akiwa uchi wa mnyama na akiwa damu.

Polisi aonekana akipeleleza lakini hakupata chochote, Rihanna anamzamisha majini.

Video hiyo ya dakika saba tayari imetazamwa mara milioni 17 katika siku 5 tu tangu ichapishwe.

Je maoni yako kuhusu video hiyo ni yapi.