Namwali mshindi wa Tuzo la Caine

Image caption Mshindi wa tuzo la uandishi la Caine, Serpell Namwali

Namwali Serpell amenyakua tuzo ni mshindi wa tuzo ya Caine ya uandishi bora barani Afrika tuzo iliyotolewa Oxford Uingereza

Namwali, raia wa Zambia ameshinda tuzo hiyo kutokana na uandishi wake mahiri wa hadithi fupi kwenye chapisho lake liitwalo ''The Sack''

Mwenyekiti wa majaji wa shindano hilo Zoe wicomb, alimtangaza Namwali kuwa mshindi wa kiasi cha pauni 10,000 hiyo jana.

Miongoni mwa waliokuwa wakiwania tuzo hilo ni Waandishi wawili wa Nigeria,wawili wa Afrika kusini na mmoja wa zambia

Mwaka jana mwandishi wa Kenya Okwiri Oduor alikuwa mshindi wa tuzo hilo ambaye sasa anaendelea kuandika riwaya yake ya kwanza.

Tuzo hii hutolewa kila mwaka kwa wanaoonyesha vipaji vyao mahiri vya uandishi kutoka Afrika, tuzo hii ikipewa jina la kumuenzi sir Michael Caine,Raia wa Uingereza, mtunzi na mcheza filamu mahiri ambaye amewahi kuonekana katika zaidi ya filamu 115.

Tuzo hizi huwahusisha waandishi wa kiafrika yaani wenye sifa ya kuwa waafrika halisi kwa kuzaliwa au uraia wa nchi za kiafrika au ambaye ana mzazi aliyezaliwa nchi za kiafrika au ana uraia wa nchi hizo.

Baadhi ya waliowahi kupata tuzo la caine ni Leila Aboulela wa sudan,Helon Habila wa Nigeria,Binyavanga Wainaina na Yvone Owuor wa Kenya.