Mwanabenki mkuu Kenya hataki kuishi kifalme

Image caption Gavana wa benki kuu akataa anasa Kenya

Gavana wa Benki kuu ya Kenya Patrick Njoroge amekataa jumba la kifahari baada ya kuteuliwa kuchukua wadhifa huo.

Suala hilo limezua mjadala miongoni mwa wakenya kutokana na uamuzi huo wa bwana Njoroge, kapera mwenye umri wa miaka 54 ambaye ni mfuasi wa dini ya katoliki wa kundi linalojulikana kama Opus Dei.

Wakenya wamezoea kuwaona maafisa wa ngazi za juu serikalini wakiishi maisha ya starehe na anasa.

Image caption Gavana wa benki kuu akataa anasa Kenya

Ni suala ambalo limezua mjadala ikikumbukwa kuwa wabunge nchini kenya walijiongezea mishahara kwa dola 3,200 chini ya miezi miwili baada ya kuapishwa mwaka 2013.

Watangulizi wake Njoroge katika Benki kuu ya Kenya waliishi katika mtaa wa kifahari wa Muthaiga yaliko pia makao ya rais wa zamani wa Kenya Mwai Kibaki na makao ya mabalozi wa Marekani na Uingereza ambapo pia walipewa magari likiwemo la kifahari aina ya Range Rover na walinzi.

Hata hivyo Njoroge aliyakataa hayo na badala yake kuamua kuishi mtaa wa wastani wa Loresho pamoja na wanachama wenzake wa Opus Dei.