Shambulio latibuka Kenya

Image caption Shambulio jingine lilitokea huko Mpeketoni mwaka jana

Shambulio hilo limefanyika karibu na Mpeketoni, ambapo wanamgambo wa Al Shabaab waliwauwa watu wapatao sitini na nane mwaka jana.

Taarifa zinasema, wasafiri katika walisikia mlipuko mkubwa uliofuatiwa na milio ya risasi.

Inasemekana kuwa washambuliaji walijaribu kulenga mabasi hayo kwa guruneti.

Maafisa wa usalama waliokuwepo walifyetua risasi kisha mabasi yaligeuza mwendo kurudi yalikotoka.

Haki miliki ya picha AP
Image caption Kenya imekabiliwa na mashambulizi mengi kutoka kwa Al Shabaab

Milio ya risasi ilisika kwa muda usiopungua dakika ishirini.

Hakuna majeruhi walioripotiwa.

Hata hivyo kaimu mkuu wa Polisi katika eneo la Pwani, Robert Kitur amekanusha kwamba hakukuwa na shambulizi la aina yoyote.

Mabasi hayo baadaye yalifika Lamu salama.

Tukio hilo limefanyika saa chache tu baada ya wapiganaji wa Al shabaab kuwauwa watu kumi na wanne katika eneo la Mandera, kaskazini mashariki mwa Kenya.