Microsoft kufuta wafanyakazi 800

Image caption Microsoft kufuta wafanyakazi 800

Moja ya kampuni kubwa zaidi duniani ya teknolojia, Microsoft, imetangaza awamu nyingine ya kupunguza wafanyakazi wake.

Kampuni hiyo ya Microsoft imesema itawafuta kazi wafanyakazi mia nane, wengi wao kutoka kwa kampuni ya simu iliyonunua mwaka uliopita ya Nokia.

Microsoft imesema kitengo hicho hakitaendelea kuwa biashara inayojisimamia, lakini sasa imejumuishwa ndani ya kampuni kubwa ili kukuza soko kwa mfumo wake wa compiuta unaoitwa Windows.

Aidha kampuni hiyo imepunguza dhamana ya kitengo hicho kilichonunuliwa kwa zaidi ya dola bilioni saba.

Simu za mkononi za Microsoft zinazotumia Windows, zimekuwa zikijaribu kushindana na simu zinazotumia mfumo wa Android na Iphone.