Samsung Galaxy 6 haijauzwa ilivyotarajiwa

Haki miliki ya picha Samsung
Image caption Samsung Galaxy 6 haikuuzwa ilivyotarajiwa

Mauzo katika robo ya pili ya mwaka katika kampuni kubwa zaidi ya simu za mkononi duniani ya Samsung huenda yasitimize malengo ya kampuni hiyo.

Kampuni hiyo ya Korea Kusini inatabiri kuwa faida yake kati ya mwezi Aprili na Juni huenda ikashuka kwa asilimia 4 ikilinganishwa na faida iliyopata mwaka uliopita .

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Faida ya kampuni ya Samsung kupungua

Kampuni ya Samsung inasema kuwa ingependa kuona mauzo yake yakiongezeka .

Haki miliki ya picha Getty
Image caption Faida ya kampuni ya Samsung kupungua

Tangu izindue simu yake mpya ya Galaxy S6 Samsung imekumbwa na matatizo ya usambazaji wa simu hizo hali ambayo pia imeathiri mauzo yake

Haki miliki ya picha AP
Image caption Samsung imekumbwa na matatizo ya usambazaji wa simu ya Galaxy S6

Imesema kuwa imetatua suala hilo na itarajia mauzo mazuri ya simu za zamani na ya sasa ya S6.

Samsung imekuwa ikikabiliwa na ushindani mkubwa kutoka kwa makampuni ya simu ikiwemo ya Apple ya nchini Marekani na Xiaomi ya China.