Marekani kufuta kazi baadhi ya wanajeshi

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Rais wa Marekani Barack Obama

Vyombo vya habari nchini Marekani vimeripoti kuwa jeshi la marekani limethibitisha kuwa na mpango wa kupunguza jeshi lake kwa kuwaachisha kazi askari wake wapatao arobaini kwa miaka miwili ijayo.

Gazeti la USA Today linasema kuwa punguzo hilo litatangazwa rasmi katika siku zijazo na punguzo hili litaweza kuathiri nafasi za askari waliopo nyumbani na walio ndani ya nchi.

Zaidi ya wafanyakazi elfu kumi na saba watapoteza kazi zao pia.Wazo la kupunguza askari lilitangazwa mwaka jana mwezi februari na katibu wa jeshi la Marekani Chuck Hagel.