Kampeni dhidi ya tarakilishi za Apple, kunani?

Image caption Staingate

Maelfu ya watumiaji wa tarakilishi za kampuni ya Apple aina ya patakilishi wameanzisha kampeni dhidi kuharibika haraka kwa vioo vya tarakilishi hizo.

Watumiaji hao wanasema kuwa vioo hivyo vinakuwa na madoa yanayoenea katika vioo hivyo.

Phi Chong, ambaye ni muhandisi wa programu za tarakilishi ameiambia BBC kwamba alilazimika kubadilisha kioo cha cha patakilishi yake mara mbili katika kipindi cha miaka miwili.

Amesema kuwa aliambiwa kwamba Apple haiwezi kufanya marekebisho ya vioo hivyo kwa mara nyingine.

Hatahivyo mmoja ya mafundi wanaobadilisha vioo hivyo wamesema kuwa hilo si jambo la kawaida.

Lakini watumiaji ambao wameathirika wana wasiwasi kwamba watalazimika kulipa ada ya kiwango cha juu ili kurekebishiwa vioo hivyo wakati mda wao wa dhamana ya kurekebishia utakapokamilika.

Mtandao unaojiita 'Staingate' sasa umebuniwa na kundi moja ambalo halifurahii majibu ya kampuni hiyo.

Baadhi yao wanasema kuwa wameambiwa kuwa watalazimika kulipa dola 800 kwa marekebisho kufanyiwa patakilishi zao.

Kundi moja la mtandao wa facebook lililobuniwa na watu wanaokabiliwa na matatizo kama hayo ya vioo limepata wanachama 1752 huku staingate ikisema kuwa imeweza kuwasiliana na zaidi ya watu 2500 kufikia sasa.