Visa vipya vya Ebola vyaripotiwa Liberia

Image caption Wimbi jipya la ugonjwa Liberia

Wimbi jipya la maambukizi lilizuka wiki iliyopita nje ya mji mkuu, lakini bado chanzo bado hakijabainika.

Wagonjwa walioambukizwa ni mvulana na msichana kutoka Nedowein, eneo ambalo mtu wa kwanza kuambikizwa katika wimbi hili alifariki wiki iliyopita.

Taarifa hizo hazikuishtua serikali.

Tayari watu kadhaa wametengwa baada ya kuonyesha dalili za virusi vya ugonjwa huo.

Wengi wao walikaribiana na mvulana mwenye umri wa miaka 17 aliyefariki.

Wengine wengi wametengwa na vikosi vya usaidizi vinakagua maeneo kuona iwapo kuna visa vingine vya watu walioambukizwa.

Wanasema wanaamini wana kila uwezo kuudhibitiugonjwa huo na kuzia kusambaa kwake katika maeneo mengine ya nchi.

Maafisa wa serikali wanachunguza uwezekano wa mbwa mmoja aliyefariki kuwa ndio chanzo.

Wakati huo huo wagonjwa wote wanne wanapokea matibabu huko Monrovia.

Kumeripotiwa visa 30 vipya vya maambukizi ya Ebola huko Liberia, Sierra Leone na Guinea wiki iliyopita.