India yakubali mualiko wa Pakistan

Image caption Viongozi wa Pakistan na India

Waziri mkuu wa India Narendra Modi amekubali mualiko kutoka kwa mwenzake wa Pakistan, Nawaz Sharif kuhudhuria mkutano wa kieneo huko Islamabad mwaka ujao.

Hii ni ziara ya kwanza ya Modi nchini Pakistan baada ya kuingia madarakani mwaka jana.

Mkutano huu ni wa kwanza kati ya viongozi hao wawili tangu Nawaz Sharif ahudhurie sherehe za kuapishwa kwa Narendra Modi Mei 2014.

Haki miliki ya picha THINKSTOCK
Image caption Ziara hiyo imetajwa kama mafanikio

Picha za mawaziri hao wawili wakuu wakisalmiana kwa mikono zimetanda katika vyombo vya habari Pakistan.

Ziara hiyo ya waziri mkuu wa India Pakistan imetajwa kama mafanikio.

Uhusiano wa hivi karibuni kati ya nchi hizo mbili jirani umeathirika baada ya Pakistan kuishutumu India kwa kuingilia kati katika masuala yake ya ndani.

India ilifutilia mbali mkutano wa kiwango cha makatibu mwaka 2104.

Kumeshuhudiwa pia uhasama katika mpaka kati ya nchi hizo mbili.