Indonesia yafunga viwanja 5 vya ndege

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Mlipuko wa Volkano

Indonesia imefunga viwanja vitano vya ndege kikiwemo kile cha Bali kufuatia kulipuka kwa volcano katika mlima wa Raung, mashariki mwa mji wa Java.

Wizara ya uchukuzi inasema kuwa hii ni kwa ajili ya usalama wa wasafiri na bado haijulikani ni lini viwanja hivyo vitafunguliwa.

Safari nyingi kati ya Australia na Bali, eneo maarufu sana kwa utalii zimakatizwa kutokana na hatari ya mvuke na majivu ya volkano hiyo.

Haki miliki ya picha bbc
Image caption uwanja wa ndege

Wataalamu wanasema kuwa huenda mlipuko huo ukaendelea kwa wiki kadhaa.