Kampuni za pombe zalalamika Kenya

Kampuni zinazotengeza pombe nchini Kenya zimelalamikia kupata hasara ya mamilioni ya dola huku kampeni ya kufunga kampuni zinazotengeza pombe haramu ikikamilika.

Watu kadhaa wamefariki kutokana na kukosa pombe hiyo wakati wa oparesheni hiyo.

Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta alitoa agizo hilo siku ya ijumaa iliopita kufuatia vifo vya watu kadhaa vilivyosababishwa na unywaji wa pombe ghafi.

Vyombo vya habari nchini Kenya vimekuwa vikionyesha picha za maafisa wa usalama wanaovamia vilabu vya pombe pamoja na kampuni za kutengeza kinywaji hicho.

Mapipa ya pombe yalimwaywa huku chupu zikivinjwa.

Image caption Kenya brew

Lakini Makundi yanayowakilisha kampuni za kutengeza pombe yanasema kuwa oparesheni hiyo ilifanywa vibaya kwa kuwa hata pombe ilio halali iliharibiwa pamoja na mali zao.

Wanadai kuwa kampuni hizo zimepata hasara za mamilioni ya dola na kuonya kwamba huenda wafanyikazi wakafutwa kazi kutokana na hasara hiyo.

Mkuu wa mawakala wanaodhibiti dawa na utumizi mbaya wa pombe wanasisitiza kuwa msako huo ni wa halali na ulifuata agizo la rais.

Na katika tukio jipya takriban watu sita wamefariki baada kukosa pombe hiyo ilio bei rahisi.

Gavana mmoja wa mkoa wa kati nchini Kenya amewaomba wakaazi kumpeleka mtu yeyote mwenye ishara za ugonjwa hospitalini.

Image caption Pombe haramu

Wakenya wengi wanaunga mkono mpango huo kwa kuwa wanasema kuwa pombe ghafi imesababisha kuongezeka kwa unywaji pombe na kuvunjika kwa familia.