Duka la West Gate kufunguliwa Kenya

Haki miliki ya picha AP
Image caption Duka la West Gate

Jumba la kibiashara la West Gate lililoko katika mji mkuu wa Kenya Nairobi linatarajiwa kufunguliwa wikendi ijayo, miaka miwili tangu wapiganaji wa Al shabaab kutoka Somalia kulivamia.

Watu sitini na saba waliuawa baada ya wapiganaji wanne wa Al Shabaab kuliteka jengo kwa siku kadhaa mnamo mwezi September mwaka wa 2013.

Kundi hilo la kigaidi bado limeendelea kufanya mashambulio ya kigaidi nchini Kenya ikiwemo shambulio dhidi ya chuo kikuu cha Garissa ambako wanafunzi mia moja na arubaini na saba waliuawa Aprili mwaka huu.