Boko Haram yashambulia Nigeria na Chad

Haki miliki ya picha EPA
Image caption Boko Haram yashambulia Nigeria na Chad

Takriban Watu 15 wameuwawa katika mlipuko uliotokea kwenye soko kuu la mji mkuu wa Chad, N'djamena.

Mwanaume aliyekuwa amevalia Burka alijilipua sokoni.

Chad na Nigeri zimeshirikiana na Nigeria, kupigana na wanamgambo hao wa kiislamu.

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Mwanaume aliyekuwa amevalia Burka alijilipua sokoni.

Wakati huohuo huko Nigeria, watu wanaoshukiwa kuwa wapiganaji Waislamu wa Boko Haram, wamefanya mashambulio ya kujitolea mhanga .

Maafisa wanasema kuwa washambuliaji wawili, walijilipua katika mji wa Maiduguri, ulioko Kaskazini-Mashariki mwa Nigeria

Haki miliki ya picha AP
Image caption Watu zaidi ya 200 wameuwawa kwenye mashambulio nchini Nigeria katika siku 10 zilizopita.

Mji huo ndio uliokuwa kitovu cha Boko Haram.

Watu zaidi ya 200 wameuwawa kwenye mashambulio nchini Nigeria katika siku 10 zilizopita.

Wandani wanasema kuwa Boko Haram imeimarisha mashambulizi haswa wakati huu wa ramadhan.