Mlipuko mkubwa waukumba mji wa Cairo

Image caption Mlipuko mkubwa waukumba mji wa Cairo

Kumetokea mlipuko mkubwa nje ya ubalozi wa Italia kwenye mji mkuu wa Misri Cairo.

Maafisa wa usalama wanasema kuwa bomu lililokuwa limetewa ndani ya gari lililipuka ambapo Takriban mtu mmoja aliuwa na wengine wannne wakajeruhiwa .

Mlipuko huo uliripotiwa kuharibu lango la ubalozi huo. Vikosi vya usalama vimekuwa vikilengwa mara kwa mara na wanamgambo tangu serikali ya rais Mohamed Morsi ipinduliwa mwaka 2013.