Islamic State yadai kushambulia Misri

Image caption Islamic State yadai kushambulia Misri

Kundi la wapiganaji wa Kiislamu la Islamic State limedai kutejkeleza shambulizi la bomu nje ya ubalozi wa Italia mjini Cairo Misri mapema jumamosi.

Shambulizi hilo lililoharibu jengo la ubalozi huo linaaminika kutekelezwa na bomu lililotegwa ndani ya gari.

Haki miliki ya picha AP
Image caption Mtu mmoja tu ndiye aliyeuawa katika shambulizi hilo.

Mtu mmoja tu ndiye aliyeuawa katika shambulizi hilo.

katika ujumbe uliotolewa muda mchache uliopita, Islamic State inawaonya waislamu wajiepushe na mijengo kama maeneo ya ubalozi kwani ndizo zinazolengwa.

Waliojeruhiwa kulingana na maafisa wa serikali ni pamoja na walinzi wa ubalozi huo na wapita njia.

Haki miliki ya picha no credit
Image caption Askari wa usalama wamelengwa mara nyingi na wapiganaji, tangu jeshi lilipompindua rais wa Muhammad Morsi

Kufuatia shambulizi hilo kubwa, serikali ya Italia imekariri kuwa haitatikiswa kamwe na ugaidi.

Askari wa usalama wamelengwa mara nyingi na wapiganaji, tangu jeshi lilipompindua rais wa Muhammad Morsi na kundi lake la the Muslim Brotherhood mwaka wa 2013.