Harrisson Ford amepata nafuu

Haki miliki ya picha Getty
Image caption Harrisson Ford amepata nafuu

Muigizaji nyota wa filamu za Hollywood Harrisson Ford ameonekana hadharani kwa mara ya kwanza tangu ahusike katika ajali ya ndege mwezi Machi.

Nyota huyo kutoka Marekani alikuwa mgeni wa heshima katika mkutano na mashabiki wa filamu ya Star Wars ulioandaliwa huko San Diego Comic-Con.

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Mabaki ya ndege aliyokuwa ndani ilipoanguka mwezi Machi

Ford mwenye umri wa miaka 72 aliwaambia maelfu wa mashabiki wake kuwa

" Mimi ni mzima wa afya.''

''Iwapo nimetembea mwenyewe hadi hapa hiyo ni ishara kuwa mimi ni mzima au sio ? aliuliza Ford

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Ford, aliyejeruhiwa mguu wake vibaya alipoanguka na ndege katika uwanja wa gofu

Ford, aliyejeruhiwa mguu wake vibaya alipoanguka na ndege katika uwanja wa gofu aliandamana na wasanii wenza walioigiza filamu ya Star Wars, Mark Hamill na Carrie Fisher.

Watatu hao waliigiza kama Han Solo, Luke Skywalker na Princess Leia katika onyesho lijalo la Star Wars, ''The Force Awakens''.

Haki miliki ya picha AFP
Image caption ''The Force Awakens'' itazinduliwa tarehe 18 Desemba.

Mashabiki sugu wa filamu hiyo walikuwa wamepiga foleni kwa siku kadhaa iliwajipatie viti vya hapo mbele karibu na jukwaa.

Wasanii wachanga katika filamu hiyo Daisy Ridley na John Boyega pia walikutana na mashabiki wao.

''The Force Awakens'' itazinduliwa tarehe 18 Desemba.