Mwanaharakati Mpalestina aachiwa huru

Haki miliki ya picha AP
Image caption Mwanaharakati Mpalestina aachiwa huru

Mwanaharakati wa Kipalestina Khader Adnan ameachiliwa kutoka gerezani na utawala wa Israeli baada ya kukubali kumaliza mgomo wa kutokula ambao ulidumu kwa zaidi ya siku 50.

Amekuwa gerezani kwa mwaka mmoja.

Alikamatwa kufuatia kuuwa kwa vijana watatu wa Israel hali iliyosababisha kukamatwa kwa wapalestina wengi.

Idara za usalama nchini Israeli zinasema kuwa bwana Adnan ni mwanachama wa kundi moja la kiislamu lakini familia yake inasema kuwa ahusiki kwenye shughuli kama hizo.