Polisi 2 wauawa na Al-Shabaab Kenya

Image caption Hii ndio mara ya kwanza kwa bomu la kutegwa ardhini kutegwa katika eneo hilo

Watu watano miongoni mwao maafisa wawili wa polisi wamefariki baada ya gari walilokuwa wakisafiria kukanyaga bomu la kutegwa ardhini.

Watano hao walikua wakielekea mjini Lamu katika Pwani ya Kenya

Kamishna wa jimbo la Garisa anasema kuwa maafisa hao walikuwa kazini wakielekea eneo la Hindi, kununua bidhaa za matumizi.

Mwandishi wa BBC aliyeko Garissa anasema kuwa gari hilo la serikali liliharibiwa vibaya katika shambulizi hilo la kwanza la aina hiyo.

Alisema kuwa bomu hilo lilikuwa limetegwa barabarani.

Haki miliki ya picha KDF
Image caption Mwezi uliopita wapiganaji 11 wa Al Shabaab waliuawa Lamu

Uchunguzi wa kwanza unaashiria kuwa hilo lilikuwa ni shambulizi la kundi la wapiganaji wa kiislamu kutoka Somalia Al Shabaab.

Mwezi uliopita jaribio la wanamgambo hao kuishambulia kambi ya jeshi la Kenya katika eneo hilo lilipelekea 11 kati yao kuuawa.

Hiyo ndiyo iliyokuwa mara ya kwanza kwa wapiganaji wa kigeni kupatikana miongoni mwa washambulizi wa kundi hilo baada ya mwili wa muingereza Thomas Evans ulipatikana.