Sierra Leone yatishwa bado na Ebola

Haki miliki ya picha BBC World Service
Image caption Wataalam wa afya dhidi ya Ebola

Maofisa wa afya nchini Sierra Leone wametahadharisha uwezekano wa kutokea maambukizi zaidi ya virusi vya ugonjwa wa Ebola ikiwa ni mwaka mmoja tangu mgonjwa wa kwanza kubainika nchini humo. Wamesema kuwa hofu ya baadhi ya watu kukataliwa na kutengwa na jamii ni moja ya sababu inayochangia kuenea kwa maambukizi hayo kwani wengi hujificha wanapokumbwa na ugonjwa huo. Hata hivyo kumekuwa na kasi ya kupungua kwa maambukizi ya ugonjwa huo katika siku za hivi karibuni ,japo kuwa katika makao makuu ya nchi hiyo Freetown hivi karibuni kumekuwa na maambukizi mapya ya ugonjwa huo. Zaidi ya watu 4000 walikufa kutokana na ugonjwa wa Ebola nchini Liberia na hivyo kuifanya nchi hiyo kuwa moja ya nchi tatu zilizoathirika na Ebola,zikiwemo Guinea na Liberia.