Akamatwa akijaribu kuuza mtoto wa miezi 3

Haki miliki ya picha Greater Manchester Police
Image caption Akamatwa akijaribu kuuza mtoto wa miezi 3

Mwanaume mmoja aliyekuwa akikusudia kuuza mtoto amekamatwa na polisi mjini Manchester.

Polisi wanasema kuwa wamemkamata bwana huyo mwenye umri wa miaka 28 karibu na soko la Barton Arcade mwendo wa saa nane u nusu majira ya Uingereza.

Polisi wanasema kuwa alikuwa na mtoto msichana anayekisiwa kuwa na miezi 3.

Aidha anasemekana kumuuliza mpita njia iwapo angependa kumnunua mtoto aliyekuwa katika kigari cha kuwakokota watoto.

Polisi waliitwa na mara moja wakamtia mbaroni kwa makosa ya kumtelekeza mtoto.

Mtoto huyo yuko chini ya ulinzi wa serikali na anasemekana kuwa yuko katika hali nzuri kiafya.

Inspekta Liam Boden anasema kuwa watamhoji kuhusiana na madai hayo huku upelelezi wa kina ukianza.