Michuano ya Kagame kuanza kutimua vumbi

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Rais wa Rwanda Paul Kagame

Michuano ya klabu bingwa Afrika Mashariki na Kati jumamosi wiki hii inaanza kutimua vumbi mjini Dar es Salaam Tanzania huku jumla ya vilabu 13 vikishiriki.

Rais wa Rwanda Paul Kagame anatarajiwa kutoa kiasi cha dola elfu 60 za marekani kama zawadi kwa washindi.

Kundi A itajumuisha timu za Yanga yaTanzania, Gor Mahia ya Kenya, Kmkm Zanzibar, Telecom ya Djibout na Khartoum- Sudani Kaskazini.

Kundi B - APR Rwanda, Al Shandy ya Sudan, LLB FC Burundi naHeegan Somalia.

Wakati kundi C - Azam ya Tanzania, Malakia ya Sudan Kusini, Adama ya Ethiopia na KCCA ya Uganda.

Hata hivyo mgawanyo wa zawadi kwa kila mshindi ni kwamba mshindi wa kwanza atajinyakulia dola elfu 30, wa pili dola elfu 20 na wa tatu dola elfu 10.