Kampuni za mbao zadaiwa kufadhili vita CAR

Haki miliki ya picha Global Witness
Image caption Ukataji miti barani Afrika

Kundi la kutetea haki la Global Witness limayalaumu baadhi ya makumpuni ya mbao barani Ulaya kwa kusaidia kufadhili vita nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati, kupitia kusaidia kusaini mikataba ya fedha nyingi na makundi ya wapiganaji.

Kundi hilo la Global Witness pia linasema kuwa muungano wa Ulaya umeshindwa kuzuia mbao haramu ambazo zinauzwa barani Ulaya.

Maelfu ya watu wameuawa miaka ya hivi majuzi nchini Jamhuri ya Afrika ya kati kwenye mzozo ambao ulisababisha kuwepo kwa mauaji ya waislamu ambao ni wachache nchini humo.