Desmond Tutu alazwa hospitalini

Image caption Askofu mstaafu Desmond Tutu

Askofu mstaafu Desmond Tutu amelazwa katika hospitali moja mjini Cape Town Afrika Kusini.

Familia yake inasema kuwa amekuwa akiugua maambukizi yasioisha na kwamba huenda akatoka hospitalini hivi karibuni.

Bwana Tutu alijiuzulu katika maisha ya umma miaka minne iliopita lakini anaendelea kusafiri maeneo mengi.

Amelazwa hosptalini mara kadhaa katika miaka ya hivi karibuni na kutibiwa saratani ya tezi dume kwa mara kadhaa.

Mapema mwezi huu yeye na mkewe waliimarisha ndoa yao baada ya kula kiapo kwa mara ya pili miaka sitini baada ya kuoana.