Nyumba ya Chris Brown yavamiwa

Image caption Chris Brown

Nyumba ya nyota wa muziki Chris Brown kutoka Marekani imevamiwa na kupekuliwa na watu watatu waliofunika nyuso zao ambao walimfungia shangazi lake ndani chumba chake kulingana na maafisa wa polisi.

Nyota huyo wa muziki wa R&B hakuwepo nyumbani kwake wakati wa wizi huo ambao ulifanyika alfajiri siku ya jumatano.

Maafisa wanasema kuwa washukiwa ambao walikuwa na bunduki waliondoka katika jumba hilo la Tarzana na fedha za kiasi kisichojulikana pamoja na vitu kadhaa vya kibinafsi.

Brown au wawakilishi wake bado hawajatoa tamko lolote kuhusu tukio hilo.

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Chris Brown na Rihanna kabla ya wawili hao kukosana

Kulingana na ripoti,nyota huyo alikuwa ameenda kujivinjari katika kilabu moja wakati wa kisa hicho

Hii ni mara ya pili ya nyumba ya msanii huyo ambaye alikuwa mpenziwe nyota wa muziki wa Pop Rihanna kuvamiwa katika kipindi cha miezi ya hivi karibuni.

Mnamo mwezi Mei,aliwasili nyumbani na kumpata mwanamke mmoja aliyedaiwa kuvunja na kuingia kupika vyakula kadhaa na kuandika ukutani kwamba anampenda msanii huyo.