George HW Bush avunjika shingo

Haki miliki ya picha AFP
Image caption George H W Bush

Aliyekuwa rais wa Marekani George HW Bush amelazwa hospitalini baada ya kuvunjika mfupa wa shingoni alipoanguka nyumbani kwake huko Maine.

Msemaji wake amesema kuwa kwa sasa yuko katika hali nzuri na kwamba kulazwa kwake huenda kukachukua muda mfupi.

Bwana Bush aliye na ugonjwa wa kutetemeka na hawezi kutumia miguu yake alisheherekea siku yake za kuzaliwa mwaka uliopita kwa kuruka angani.

Alilazimika kwenda hospitalini mwishoni mwa mwaka uliopita akiwa na tatizo la kupumua.

Msemaji huyo Jim Grath amesema kuwa Bush huyo ambaye ndiye mkubwa miongoni mwa marasi wanne wa zamani wa Marekani kutoka familia hiyo atalazimika kuvaa kifaa cha kuzuia shingo kutokana na kuanguka kwake hapo siku ya jumatano.