Obama:Maafikiano na Iran yataleta amani

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Makubaliano ya mpango wa Iran wa Nuklia

Rais Barrack Obama wa Marekani, ameshinikiza kuwa muafaka ulioafikiwa siku ya Jumanne kuhusu mpango wa nuklia wa Iran, umetoa fursa ya kipekee maishani ya kutaka kuwepo kwa mahala salama pa kuishi, ulimwenguni.

Shughuli za kinuklia za Iran, zitatizamwa kwa uangalifu mkubwa, ili taifa hilo liondolewe vikwazo vya kiuchumi.

Muafaka huo ulikosolewa vikali na wanasiasa wa chama cha Republican nchini Marekani huku Waziri mkuu wa Isareli, akiupuuzilia mbali na kusema kuwa ni makosa makubwa.