Afungwa miaka 8 kwa kumuoza bintiye

Image caption Jaji wa mahakama

Raia mmoja wa Australia ambaye alipanga ndoa ya kiislamu li kumuoza bintiye mdogo mwenye umri wa miaka 12 amehukumiwa miaka minane jela.

Mwanamume huyo mwenye umri wa miaka 63 alipatikana na mwanamume raia wa Lebanon mwenye umri wa miaka 26 akimuoza bintiye kwake, huku akisema kuwa hakutaka kumuona bintiye akitenda dhambi kwa kufanya ngono nje ya ndoa.

Alipatikana na hatia mwezi Aprili kwa kumnadi mtoto kuhusika katika vitendo vya ngono kinyume na sheria.

Mapema mwaka huu mume huyo alihukumiwa kifungo cha miaka saba na nusu kwa kumnyanyasa kijinsia mtoto huyo.

Msichana huyo mdogo analindwa na serikali.