Ibada ya Eid yakumbwa na milipuko Nigeria

Haki miliki ya picha AP
Image caption Mlipuko

Jeshi nchini Nigeria linasema kuwa takriban watu 11 wameuawa kwenye mashambulizi mawili ya kujitoa mhanga kwenye mji ulio kaskazini mashariki mwa nchi wa Damaturu.

Wanasema kuwa washambuliaji wote walikuwa ni wanawake , mmoja mwenye mri mkubwa na mwingine mwenye umri wa miaka kumi.

Ripoti zingine zinasema kuwa idadi ya waliokufa ni kubwa.

Mashambulizi mengine yalifanyika kwenye maombi ya kusherehekea siku kuu ya Eid ul Fitr ya kumaliza mwezi mtukufu wa Ramadhan.

Mashambulizi kama hayo hulaumiwa kwa kundi la kiislamu la Boko Haram ambalo limeongeza mashambulizi yake tangu rais Muhammadu Buhari aingie madarakani.