Milipuko mitano yalikumba eneo la Gaza

Image caption Milipuko Gaza

Takriban milipuko mitano iliyotokea katika ukanda wa Gaza imeharibu magari ya wanachama wa kundi la Hamas na makundi mengine ya Jihad

Haijabainika ni nani alihusika na mashambuli hayo.

Lakini wadadisi wanasema kuwa huenda ni makundi madogo yanayolipinga kundi la hamas ndiyo yaliotekeleza mashambulizi hayo.

Shambulizi hilo lilifanyika kwenye mtaa mmoja katika mji wa Gaza ambapo vikosi vya Hamas hivi majuzi vilimuua mwanamgambo aliyeunga mkono kundi la Islamic State.