KHAMENEI:Iran haitabadili sera

Haki miliki ya picha AP
Image caption KHAMENEI:Iran haitabadili sera

Kongozi mkuu nchini Iran Ayatollah Khamenei amasema kuwa makubaliano kuhusu mipango ya nyuklia yaliyoafikiwa na mataifa makubwa duniani wiki iliyopiya hayawezi kubadili sera za Iran eneo la mashariki ya kati.

Akizungumza kupitia kwa runinga ya taifa kuadhimisha kumalizika kwa mwezi mtukufu wa Ramadhan, Ayatolla alisema kuwa Iran itaendelea kuwaunga mkono washirika wake eneo hilo wakiwemo serikali ya rais Bashar al Assad nchini syria, waasi wa Houthi nchini Yemen na wanamgambo wa Hamas katika utawala wa Palestina.

Amesema kuwa hakutakuwa na majadiliano yoyoye na marekani ambayo imekubali kuiondolea vikwazo vya kiuchumi ilivyoiwekea Iran ikilenga kufuatilia kwa makini mipango ya nyuklia ya nchi hiyo.