Takriban watu 100 wauawa Iraq

Haki miliki ya picha AP
Image caption Takriban watu 100 wauawa Iraq

Inahofiwa kuwa takriban watu 100 wakiwemo watoto kadha wameuawa kwenye shambulizi la bomu kwenye soko moja lenye shughuli nyingi mashariki mwa Iraq

Shambulizi hilo ambalo lilitokea katika mji wa Khan Bani katika mkoa ulio mashariki mwa nchi wa Diyala lilitokea wakati watu walikuwa wakisherehekea kumalizika kwa mwezi mtukufu wa Ramadhan.

Polisi walisema kuwa mshindo wa mlipuko huo uliangusha nyumba kadha na miili ilikuwa bado inaondolewa kutoka kwa vifusi.

Hakuna kundi lililotangaza kuhusika.