IS yadaiwa kutumia gesi ya sumu Syria

Haki miliki ya picha
Image caption Wapiganaji wa islamic state

Ripoti kutoka kaskazini mwa Syria, zinasema kuwa wapiganaji wa Islamic State, wametumia gesi ya sumu kushambulia askari wa Ki-kurd.

Wanaharakati wanaochunguza vita vya Syria, Wakurd na wenye makao Uingereza wanasema hayo yalitokea mwisho wa mwezi uliopita,katika mji wa Hasakeh.

Wanasema kuwa makombora yasiyokuwa ya kiufundi, yalitoa gesi ya manjano, iliyonuka vibaya.

Waliokuwako karibu walisikia kichefuchefu, na waliwashwa macho na koo.

Lakini hakuna mtu aliyeumia vibaya.

Maafisa wa Kikurd wanasema hawajui gesi hiyo ilikuwa ya aina gani, lakini wanaishutumu IS, kuwa siku za nyuma, ilitumia gesi ya chlorine kama silaha.