Jasusi wa Korea Kusini ajitoa uhai?

Haki miliki ya picha THINKSTOCK
Image caption Udukuzi wa mitandao

Mfanyikazi wa shirika la ujasusi la Korea Kusini amepatikana akiwa amekufa huku kashfa ya kisiasa kuhusu udukuzi wa simu ikiendelea.

Alijiua na kuwacha kijikaratasi kilichokuwa kikizungumzia mfumo wenye utata ambapo kifaa cha uchunguzi kinawekwa kwenye simu za mkononi na kompiuta.

Kwenye kijikatarasi hicho anakanusha madai kuwa serikali ilikuwa imetumia programu hiyo kuwachunguza watu nchini Korea Kusini.

Lakini alikiri kuwa aliharibu mifumo ya ujasusi ya maajenti wa Korea Kaskazini.

Serikali imesema kuwa ilikua na lengo la kuharibu uwezo wa vita vya mitandao dhidi ya Korea Kaskazini.