UNESCO:Uharibifu wa Timbuktu kuchunguzwa

Image caption Timbuktu

Shirika la elimu, utamaduni la umoja wa mataifa UNESCO limeiomba mahakama ya kimataifa ya uhalifu wa kivita kuchunguza uharibifu wa maeneo ya kale ya mji wa Timbuktu nchini Mali ulioendeshwa na wanamgambo wa kiislamu ambao walilidhibiti eneo la kaskazini mwa nchi mwaka 2012.

Mkurugenzi mkuu wa UNESCO Irina Bokova amesema kuwa kuharibiwa kwa maeneo ya kitamaduni ni kitendo cha uhalifu wa kivita.

Maeneo 16 ya kale ya kiislamu ya hadi karne za 15 na 16 yaliharibiwa na maelfu ya kumbukumbu za kale kupotea

UNESCO imeanzisha mradi wa kuyakarabati maeno hayo.