Saudi Arabia yakamata I-S wengi

Saudi Arabia imefanya operesheni kadha dhidi ya IS mwaka huu Haki miliki ya picha saudi IS

Wakuu wa Saudi Arabia wanasema katika operesheni zao za karibuni, wamewakamata watu zaidi ya 430 wanaoshukiwa kuwa wafuasi wa kundi la Islamic State.

Wizara ya mambo ya ndani ya nchi ilisema kuwa I-S ilikusudia kuleta mtafaruku na kwamba njama kadha zimezimwa.

Baadhi ya njama zilikuwa kulenga ubalozi mmoja, kuuwa askari wa usalama, na kufanya mashambulio ya kujitolea mhanga kwenye misikiti.

I-S imesema kuwa ilihusika na mashambulio mawili ya mabomu dhidi ya misikiti ya Shia, mashariki mwa nchi mwezi wa May.

Watu 25 waliuwawa.

Wakati huohuo, Mflame Salman wa Saudi Arabia amefanya mazungumzo na kiongozi wa kundi la Wapalestina la Hamas, Khaled Meshaal, ambaye alikwenda Makka kwa hija ndogo.

Ni miaka mine tangu mfalme wa Saudia Arabia, Mfalme Abdullah, mara ya mwisho kutangaza kuwa amefanya mazungumzo na kundi hilo linaloongoza Gaza.

Hamas kawaida inashikamana na Iran lakini iliikera serikali ya Iran ilipounga mkono wapiganaji wa Syria dhidi ya maadui wa wapiganaji hao, yaani Rais Bashar al-Assad.