Yemen:Vita vikali vyaendelea mjini Aden

Haki miliki ya picha AP
Image caption Waasi wa Houthi nchini Yemen

Ripoti kutoka Yemen zinaarifu kuwa mapambano makali yanaendelea katika mtaa mmoja wa mji wenye bandari ya Aden, ambako wapiganaji wa Houthi, wanapambana na askari wa serikali, na wanaosaidiwa na Saudi Arabia.

Upande wa serikali umesonga mbele sana katika mapigano ya karibuni.

Umetangaza kuwa Aden imekombolewa, na mawaziri zaidi wa serikali ya rais Hadi, ilioko uhamishoni, wamerudi mjini humo.

Mmoja wao alisema, vikundi vichache vilivyozingirwa, vinakataa kujisalimisha.