Nigeria: afisa wa usalama apekuliwa

Usalama Maiduguri, Nigeria Haki miliki ya picha EPA

Wakuu wa Nigeria wanasema kuwa wamevamia mara kadha nyumba za mshauri wa usalama wa zamani.

Idara ya usalama wa taifa imesema kuwa uvamizi huo umefanywa kufuatana na taarifa za upelelezi za kuaminika, zilizomhusisha Mohammed Sambo Dasuki na mipango ya kufanya uhalifu dhidi ya taifa.

Ilisema kuwa bunduki na zana nyengine za kijeshi zilikutikana kwenye nyumba hizo zilizovamiwa.

Bwana Dasuki alitolewa juma lilopita katika kazi yake ya kuishauri serikali kuhusu usalama.