Ulanguzi katika soka :BBC imegundua

Image caption klabu ya Champasak matatani kwa ulanguzi wa wachezaji

Wachezaji wa Afrika,miaka 14 wanasafirishwa kiharamu barani Asia, BBC yagundua.

Wanalazimishwa kusaini mikataba kinyume cha sheria.

Wachezaji 6 bado wako katika klabu ya Champasak United baada ya klabu hiyo mjini Laos kuwachukua watoto 23 kutoka Afrika magharibi kuwapeleka chuo bandia cha soka mwezi Februari.

Kanuni za FIFA zimeharamisha kuwasafirisha watoto chini ya miaka 18 kwa klabu za kigeni au chuo cha soka.

"FIFA inawasiliana na mashirikisho kadhaa kukusanya maelezo na kuchunguza suala hilo ili ihifadhi maslahi ya watoto,'' amesema afisa wa FIFA.

Haki miliki ya picha BBC World Service
Image caption wachezaji wajikuta katika dhiki Laos

Inadaiwa kuwa klabu ya Champasak United inatarajia kufaidi kwa kuwauza wachezaji hao baadae.

Ikiwa na makao yake mji wa kusini wa Pakse, klabu hiyo imekanusha madai yote.

Kinyume kabisa na sheria za shirikisho la soka duniani, kalbu hiyo imewashirikisha wachezaji wadogo kati ya miaka 14 na 15 katika ligi za msimu huu.

Mchezajiwa miala 14 wa Liberia,Kesselly Kamara, hata amewahi kufunga bao.

Kabla ya kuchezea timu hiyo ya wakubwa, anasema kuwa alilazimishwa kusaini mkataba wa miaka 6.

Licha ya kusaiani mkataba huo, na kuahidiwa mshaharana makao, Kamara anasema kuwa hajawahi kulipwa na amelazimika kulala sakafuni katika uwanja - kama walivyofanya pia vijana wengine waliosafiri naye.

"ilikuwa mbaya sana, kwasababu huwezi kuweka watu 30 kulala katika chumba kimoja,'' Kamara, ambaye sasa anachezea klabu moja nyumbani Liberia, ameambia BBC.

Wote walisafiri kujiunga na chuo cha mafunzo ya soka cha Asia 'IDSEA Champasak' baada ya kupata mualikko kutoka kwa mchezaji wa zamani wa kimataifa kutoka Liberia Alex Karmo, ambaye kisha alikuwa kapteni wa klabu hiyo.

Mualiko huo ulipokewa kwa hamu kwa kuwa Liberia haina chuo chake cha mafunzo ya soka, licha ya kuwa nchi ya pekee Afrika kuwahi kutoa mchezaji bora wa FIFA duniani- George Weah (1995).

Haki miliki ya picha BBC World Service
Image caption Alex Kamara anadai kuwa kocha wa watoto

"Ni chuo tapeli ambacho hakijawahi sajiliwa kisheria ,'' amesema mwandishi wa michezo nchini Liberia na mhamasishaji wa soka Wleh Bedell, ambaye alisafiri na kundi hilo mjini Laos mwezi Februari kisha akarejea nyumbani.

"Ni chuo ambacho hakina mkufunzi, wala daktari. Karno ndiye aliyekuwa kocha, meneja biashara, kila kitu ni yeye. Ni ajabu kweli.''

Haki miliki ya picha BBC World Service
Image caption watoto wa Afrika magharibi waliohadaiwa

Kufuatia shinikizo kutoka kwa FIFA, na Umoja wa wachezaji duniani FIFPro, Champasak ililazimika kuwarudisha watoto 17 kutoka kundi lililosafirishwa na akiwemo Kamara miongoni mwao, miezi 3 iliyopita.

Lakini wachezaji 6 walikataa kurudi.

FIFPro inasema kuwa hao 6 wamesaini mikataba waliyoletewa na Karmo, anayejidai kuwa 'meneja wa wachezaji kutoka Afrika wa klabu ya Champasak' na rais wa klabu Phonesavanh Khieulavong.

Haki miliki ya picha BBC World Service
Image caption mkataba waliosaini

Hii imesababisha Champasak kutowalipa vijana hao chochote huku ikiitisha matakwa yasiyowezekana iwapo vijana hao watataka kuondoka klabu hiyo.

Hata hivyo Karmo amesisitiza kuwa wachezaji hao wamalishwa milo mitatu kwa siku na wanalipwa kila mwezi.

"Hatuwezi kuwapa watoto hao mikataba ya kitaalamu,ila ni mikataba inayoruhusu kuwapa marupurupu,'' Khieulavong ameambia BBC.

Khieulavong wala Karmo hawakukanusha kuwepo watoto wadogo katika vyuo hivyo japo raia huyo wa Liberia anadai kuwa ni kijana mmoja wa miaka 16 - kutoka Guinea.

BBC imegundua kuwa kuna watoto 5 zaidi kutoka Liberia katika klabu hiyo.

Pamoja na wachezaji wakubwa 8 (6 kati yao wa Liberia, mmoja wa Ghana na mmoja wa Sierra Leone) wote wanaishi katika ''mazingira ya kutamausha'' kama anavyoeleza Bedell.

Kwa miezi 5 wamekuwa wakilalia magodoro membamba katika chumba kimoja ambachi hakina hata madirisha wala konji katika mlango wake.

"ni vigumu sana kuishi katika chumba ambacho hakina madirisha. Ilifanya kualal kuwa vigumu sana kwakuwa saa zote unafikiria maisha yako,'' amesema Kamara.

"Wachezaji wamewekwa katika mazingira sawa na yale ya wakati wa vita vya ndani vya Liberia ambapo watu walilazimika kukimbia makwao n akutafuta hifadhi katika majengo tupu na ukumbi,'' Bedell, ambaye alishuhudia vita vya ndani nchini mwake mwaka wa 1989-96 na 1999-2003, ameambia BBC

Uhuru wa wachezaji hao ulibanwa zaidi baada ya visa zao kumalizika mnamo mwezi Machi na kulazimika kuishi kama wahamiaji haramu.

Haki miliki ya picha BBC World Service
Image caption watoto hawana visa wala vibali vya kufanya kazi

Sasa wana matumaini ya kupata vibali vya kufanya kazi, japo hili ni vigumu kwa kuwa wote hawajafika umri.

Karmo, ambaye anasisitiza kuwa alimlipa Kamara, amekiri kuwa wachezaji 14 wa Afrika kweli hawana vibali vya kuajiriwa, lakini amehakikisha kuwa wanazo stakabadhi za kuishi mjini Laos.

"Hakuna anayeishi knyume cha sheria. Kila mmoja anacho kibali,'' ameambia BBC.

Huku klabu hiyo ikishikilia pasi zao za usafiri tangu kuwasili kwao, ni nadra sana kwa vijana hao kutoka nje ya uwanja huo ambako wanaishi na kufanya mazoezi mara mbili kwa siku.

Lakini licha ya masaibu yao, sio kila mtu anawataka watoke Laos.

"Mimi sitaki arudi nchini Liberia hadi afaulu ndoto yake,'' amesema Bella Tapeh, zazi wa mmoja wa vijana wa miaka 17 ambaye bado yupo Pakse.

Baadhi ya vijana waliorudi nchini Liberia wameambia BBC kuwa hawakulishwa vizuri, walilipwa kwa nadra sana na hawakupokea matibabu kutoka kwa klabu hiyo licha ya kuambukizwa malaria na homa ya tumbo kwasababu ya hali ilivyo.

Mmoja hata ameelezea kuwepo katika klabu hiyo ya Champasak, iliyozinduliwa mapema mwaka huu kuwa 'sawa na utumwa'.

"Hii ni hali ya dharura sana,'' Stephane Burchkalter,afisa wa FIFPro ameambia BBC.

"Inashtusha kwa FIFPro kuwa klabu kutoka Laos, ambayo - bila kuikosea heshima - ni nchi ndogo sana ya soka imewavutia wachezaji (ISHIRINI) walio chini ya umri kutoka Liberia bila FIFA kujua.''

Katika taarifa, FIFPro imesema kuwa wanashuku hiki ni kionjo tu ya hali ilivyo.

Shirika moja lisilo la kiserikali (<http://www.footsolidaire.org/>), linakisia kuwa takriba vijana wachezaji wa soka 15,000 wa umri mdogo wanasafirishwa kutoka Afrika Magharibi kila mwaka - wengi wao kinyume cha sheria.

FIFPro pia imetoa wito kwa FIFA ichukua hatua dhidi ya shirikisho la soka la Laos ambalo kufikia ssa limesindwa kuiadhibu klabu ya Champasak kwa kukiuka kanuni zake.

Ushahidi wa vilabu vinavyovunja sheria za kuwasajili wachezaji chini ya umri wa miaka 18 ni nadra sana japo klabu ya Barcelona imekutikana na hatia hii na imepewa marufuku ya miezi 14 ya kuwanunua wachezaji.

Wakati uo huo wazazi wa watoto 12 wamejikuta katika matatizo ya kifedha baada yakuchukua mikopo kugharamia $550 kuwasafirisha wanao mjini Laos. Mojawepo ya kesi hizo iko mikononi mwa polisi.

Kuna nafasi tatu pekee ambapo sheria hii ya FIFA ya kuwasafirisha wachezaji chini yamiaka 18 inaweza kutumika na zote hazitumika hapa.