Hatimaye mabenki yafunguliwa Ugiriki

Image caption Mabenki yafunguliwa Ugiriki

Mabenki Nchini Ugiriki yanafunguliwa leo kwa mara ya kwanza katika mkipndi cha majuma matatu.

Kuna milolongo mirefu kwa sasa nje ya mabenki hayo, pale bunge la taifa hilo lilipopitishia masharti magumu juma lililopita kama sehemu ya kutatua matatizo yake ya kifedha.

Haki miliki ya picha EPA
Image caption Foleni ndefu zimeonekana kote nchini humo

Baadhi ya masharti yangali pale pale, ikiwemo viwango vya fedha ya mtaji kutoka mataifa ya ulaya.

Badala ya kutoa fedha kila siku kulingana na kiwango kilichowekwa sasa raia wanaweza kutoa kiwango cha Euro 420 mara moja kwa juma.

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Ushuru wa mauzo umeongezwa hasa kwa bidhaa na huduma

Ushuru wa mauzo umeongezwa hasa kwa bidhaa na huduma ukiwemo nauli ya usafiri na bei ya chakula mikahawani.

Jana Jumapili, Rais wa Ufaransa Francois Hollande, alisema kuwa shida nchini Ugiriki inafaa kutoa fursa kwa mataifa ya bara Ulaya kubuni serikali moja ya muungano.