Ashinda Scrabble bila kujua lugha

Image caption Ashinda mashindano ya dunia ya mchezo wa Scrabble kwa Kifaransa bila kujua lugha hiyo

Raia wa New Zealand asiyezungumza kifaransa hata neno moja ameshinda mashindano ya dunia ya mchezo wa scrabble, kwa lugha hiyo.

Waandaaji wa mashindano hayo wanasema Nigel Richard alimshinda mpinzani wake kutoka Gabon ambaye ni mzungumzaji mzuri wa kifaransa katika fainali zilizofanyika hapo jana.

Richard aliripotiwa mwanzoni mwa mwaka huu kuwa aliweza kujifunza kamusi na mnyambuliko wa maneno ya kifaransa ndani ya wiki tisa, lugha ambayo ndiyo iliyotumika mwaka huu.

Mashindano yaliyopita yalikuwa ya lugha ya kiingereza na yalifanyika New Zealand, mahali ambapo Mshindi huyo ametoka na kwa sasa anaishi Malaysia.