Mabadiliko ya muda wa kulala na saratani

Haki miliki ya picha spl
Image caption Ugonjwa wa Saratani

Mabadiliko katika mfumo wa kulala unaweza kusababisha mtu kupata saratani ya Maziwa.

Hiyo ni kwa mujibu wa ripoti ya wanasayansi juu ya athari ya kazi za zamu kiafya.

Utafiti unaonesha kuwa wanawake wana hatari kubwa ya kupata tatizo hilo na kwamba ni tatizo kubwa kwa wafanyakazi wanaofanya kazi za zamu na wahudumu wa ndege. Matatizo hayo yanakuja kutokana na kwamba mabadiliko ya muda wa kulala unavuruga mfumo mzima wa mwili kupumzika, hivyo huongeza hatari za kupata magonjwa.

Hata hivyo sababu nyingine zinazochangia ni kiwango cha shughuli anazofanya mtu au kiasi cha vitamin D wanachopata.

Vimelea vya mtu kupata saratani huwa vinachelewa kwa saa 12 kwa wiki, kwa mtu kuvipata katika mwaka na kawaida wanapata uvimbe baada ya wiki 50 lakini kwa wale wenye mpangilio mzuri wa kulala uvimbe hjitotokeza wiki nane kabla.

Utafiti unaonesha mkanganyiko wa mwanga na giza unaweza kusababisha mtu kupata saratani. Kwa Ujumla, mtu kufanya kazi za zamu wakati wote kunaleta msongo wa mawazo na kupunguza mwili.