Nakala za kale zaidi za Koran - UK

Image caption nakala za kale za Koran

Chuo kimoja kikuu nchini Uingereza kimesema kuwa utafiti waliofanyia nyaraka za zamani katika maktaba yake, umeonesha kuwa huenda zikawa nakala za zamani sana duniani za koran. Watafiti katika chuo cha Birmingham wanasma kuwa walishangazwa sana walipogundua kupitia uchunguzi wa miale ya radiocarbon kuwa nyaraka hizo kutoka kitabu kitakatifu cha waislamu Koran, zina umri wa zaidi ya miaka 1300,

wanasema kuwa mwandishi wa nyaraka hizo huenda alikutana ana kwa ana na mtume Muhammadau alikuwa miongoni mwa wanafunzi wake.

Nyaraka hizo ni miongoni mwa maelfu zingine za kale kutoka mashariki ya kati ambazo zilimilikiwa na mwana historia mzawa wa Iraq, Alphonse Mingana, aliyekabidhi kwa chuo kikuu hicho cha Birmingham katika miaka ya ishirini.