Msanii wa vichekesho Bill Cosby matatani

Bill Cosby Haki miliki ya picha AP
Image caption Wakili wa asema yuko tayari kumhoji Cosby kwa mashtaka ya ngono

Msanii wa vichekesho wa Marekani Bill Cosby ameshindwa kuzuia kesi ya shutuma za kumyanyasa kingono msichana mwenye umri wa miaka 15- katika jumba la kifahari la Playboy mjini Los Angeles mnamo mwaka 1974.

Mahakama kuu ya California imekataa ombi lake la kutaka dhidi yake iliyowasilishwa na Judy Huth iangaliwe upya - hii ikimaanisha kuwa wakili wa msichana anaweza sasa kumhoji bwana Cosby kwa kulingana na kiapo.

Cosby mwenye umri wa miaka 78 anakabiliwa na kesi kali ya unyanyasaji wa kingono linalodaiwa kutekelezwa miongo kadhaa.

Wakati wote amekuwa akisistiza kuwa hana hatia na hajawahi kushtakiwa kwa uhalifu.

Haki miliki ya picha AP
Image caption Cosby amekua akisisitiza kuwa hana hatia yoyote

Bi Huth anadai kwamba Bwana Cosby alimlewesha kwa pombe kabla ya kumnyanyasa ki ngono.

Wakili wake,Gloria Allred , alielezea hatua hiyo ya mahakama kama "ushindi mkubwa" na akasema ameazimia kumhoji msanii huyo mwezi ujao.

Mapema wiki iliyopita idara ya polisi ilithibitisha kwamba inachunguza ''malalamiko fulani dhidi yake''

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Bill Cosby alikua kipenzi cha wengi miaka ya 1980 na 90

Bwana Cosby alikua msanii maarufu zaidi wa television matika miaka ya 1980 na 90.

Makumi kadhaa ya wanawake wamemshitaki msanii huo wa vichekesho kwa kuwanyanyasa kingono , lakini mengi kati ya madai yao hayakua na ushahidi wa kisheria.